Mpanda FM

Mpanda yajipanga kutunga sheria ili kulinda utamaduni

7 February 2025, 1:23 pm

Picha ya mstahiki meya wa halmashauri ya Mpanda Haidary Sumry. Picha na Anna Mhina

“Jamii ipatiwe elimu na kushirikishwa katika kutunga sheria ndogondogo”

Na Restusta Nyondo

Halmashauri ya manispaa ya Mpanda imesema kuna haja ya kutunga sheria ndogondogo za kulinda na kuhifadhi utamaduni usioshikika ikiwemo lugha za asili na kuuendeleza kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadaye .

Hayo yamesemwa na mstahiki meya wa manispaa ya Mpanda Haidary Sumry  baada ya kupatiwa mafunzo na Shirika la vyombo vya habari kwa maendeleo ya jamii (TAMCODE) kupitia mradi uliofadhiliwa na Shirika la UNESCO- Alwaleed Philanthropies ambapo amesema ni wakati sasa kuanza kurithisha tamaduni za jamii mkoani hapa.

Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda, Tulinawo Nswila amesema kuwa ili kuendelea kuyaenzi masuala ya utamaduni ni lazima jamii ipatiwe elimu na kushirikishwa katika kutunga sheria ndogo zinazohusisha masuala ya uhifadhi wa utamaduni.

Sauti ya Tulinawo Nswila

Mratibu wa mradi huo kutoka Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii (TAMCODE) ambao ni watekelezaji wa mradi huo, Wakili Philomena Mwalongo amesema mjadala huo unalenga kuibua na kukuza nafasi za ajira kwa wananchi hususani vijana na wanawake.

Sauti ya Wakili Philomena Mwalongo

Mafunzo hayo yaliwakutanisha meya wa manispaa ya Mpanda, Kaimu Mkurugenzi wa halmashuri, madiwani na wataalamu kutoka katika halmashauri hiyo.