

4 February 2025, 2:35 pm
Mstahiki meya wa halmashauri ya Mpanda akizindua tractor. Picha na Rachel Ezekia
“Wakulima wanapaswa kutumia zana bora za kilimo ili kupata mavuno mengi”
Na Rachel Ezekia
Wakulima Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kulima kilimo chenye tija kwa kufuata kanuni na taratibu za kilimo bora kama ambavyo wataalam wa kilimo wanavyoshauri.
Wito huo umetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry katika zoezi la kukabidhi katapira kwa mkulima wa manispaa ya Mpanda kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa Passleasing amesema kuwa wakulima wanapaswa kutumia zana bora za kilimo pamoja na utunzaji wa maeneo ya kilimo.
Kilo Lusewa ni Mkurugenzi Mkuu wa Passsleasing amebainisha kuwa katika mkoa wa Katavi wametenga kiasi cha shilingi billion 3 ili kuwanufaisha wakulima na pembejeo bora za kilimo ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serikali kutoa elimu ya matumizi bora ya zana za kilimo.
Kwa upande wake mkulima aliyekabidhiwa katapira hilo Samwel Nzobe ameeleza ambavyo hapo awali kilimo chake kilivyokuwa pamoja na matarajio ya kuwa na kilimo cha kisasa chenye tija baada ya kupata katapira hilo.