

4 February 2025, 1:46 pm
Picha ya viongozi walioshiriki sherehe za kilele cha wiki ya sheria. Picha na Anna Mhina
“Malipo madogo hayakizi mahitaji”
Na Lilian Vicent
Chama cha mawakili Tanzania (TLS) mkoani Katavi kimelalamikia malipo madogo ambayo hayakidhi mahitaji
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa mwenyekiti wa chama cha mawakili mkoa wa Katavi wakili Nassoro Ntenga katika kilele cha wiki ya sheria nchini.
Aidha hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Katavi Gway Sumaye amekidai mahakama wameanza kutazama sehemu ya mipango muhimu ya utekelezaji wa dira ya maendeleo ya miaka 25 ijayo.
Katika hatua nyingine wakili Nassoro Ntenga ametoa wito kwa watu wasiokuwa mawakili wanaofanya shughuli za uwakili (Vishoka) kuacha kufanya kazi hiyo ili wananchi wasiweze kuharibiwa mashauri yao mahakamani.