

31 January 2025, 7:50 pm
Picha ya baraza la madiwani wa halmashauri ya Mpanda. Picha na Edda Enock
“Madiwani walalamikia kampuni za uchimbaji madini”
Na Edda Enock
Baraza la madiwani manispaa ya Mpanda mkoani Katavi limelalamikia kampuni za uchimbaji madini ambazo zinafanya shughuli za uchimbaji pembezoni mwa vyanzo vya maji na kupelekea uharibifu wa mazingira ambao umeleta athari kwa wananchi wa maeneo hayo.
Madiwani wametoa malalamiko hayo katika kikao Cha baraza hilo ambapo mbali na athari zinazojitokeza pia wamehoji halmashauri inavyofaidika na uchimbaji huo ambao unafanywa na Raia wa kigeni kutoka China.
Akijibu malalamiko hayo kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda amesema vibali vya kuchakata madini maeneo ya mito vinatolewa na mamlaka tatu wakiwemo watu wa bonde ambapo amesema kufuatia uharibifu uliofanyika walilazimika kuwapiga faini wahusika na kuzuia kuendelea kwa shughuli hizo lakini walikaidi agizo hilo huku meya wa manispaa hiyo Haidari Sumri akigiza kamati ya mipango miji kwenda kutembelea maeneo hayo na kujionea athari zilizopo.