

31 January 2025, 7:36 pm
Picha ya mwenyekiti wa baraza la ardhi na nyumba Katavi Gregory Kalashani. Picha na Anna Mhina.
“Wananchi mkoani Katavi wameomba elimu ya ardhi itolewe zaidi”
Na Liliani Vicent
Baadhi ya wananchi mkoani Katavi wametoa maoni yao kuhusiana na hatua za kuchukuliwa na serikali ili kupunguza migogoro ya ardhi.
Wametoa maoni hayo wakati wakizungumza na Mpanda redio FM ambapo wametaka elimu iendelee kutolewa kwa wananchi.
Gregory Kalashani ni mwenyekiti wa baraza la ardhi na nyumba amesema wananchi wengi wamekuwa hawafuati taratibu za kufungua kesi ya migogoro ya ardhi kwa kupitia fomu maalumu.
Wananchi wameshauriwa kufika katika Mahakama na vyombo maaalum vya kutatua migogoro ya ardhi ikiwemo Baraza la Kijiji la ardhi ,Baraza la kata ,Baraza la ardhi na nyumba la wilaya, mahakama kuu na mahakama ya rufaa ili kupata suluhu ya migogoro ya ardhi.