Mpanda FM

Wapishi wa migahawa watakiwa kuzingatia usafi

17 January 2025, 10:05 am

Mama muuza mgahawa akiwa katika mgahawa wake. picha na Anna Milanzi

Uchafu wa mazingira katika migahawa  unaweza  kusababisha magonjwa ya matumbo pamoja na kipindupindu

Na Leah Kamala – Katavi

Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Wamewataka  wamiliki na wapishi wa migahawa kuzingatia usafi  ili kujiepusha na ugonjwa wa Kipindupindu.

Wakizungumza na Mpanda Redio FM wamesema kuwa  uchafu wa mazingira katika migahawa  unaweza  kusababisha ugonjwa wa kipindupindu kuenea kwa haraka na kuiomba serikali kusimamia sheria ili usafi uzingatiwe.

Sauti za wananchi wakizungumzia hali ya usafi katika maeneo ya migahawa

Daktari Gabriel  Elias Lukubigwa Mratibu wa tiba  Manispaa ya Mpanda  amesema kuwa  wamejipanga kuwatumia maafisa afya kupita  maeneo yenye migahawa  kuangalia kama wanazingatia kanuni za afya na lishe.

Sauti ya Daktari Gabriel  Elias Lukubigwa Mratibu wa tiba  Manispaa ya Mpanda

Kwa upande wake  mkuu wa wilaya ya mpanda mkoani hapa Jamila Yusuph Kimaro amesema uuzaji wa vyakula maeneo ya shule haurusiwi ambapo wafanyabiashara  wanapaswa kutafuta maeneo tofauti na shule kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa kipundupindu.

Sauti ya Jamila Yusuph Kimaro wa wilaya ya Mpanda