Jamii yatakiwa kufanya mazoezi, kupunguza kula vyakula vya mafuta
16 January 2025, 1:26 pm
“Ulaji wa chakula cha mafuta mara kwa mara ni hatari kwa afya lakini pia mwili wa binadamu unahitaji mazoezi ili uzidi kuimarika na kuepuakana na magonjwa“
Na Roda Elias -Katavi
Wananchi mkoani Katavi wameshauriwa kufanya mazoezi na kupunguza kula vyakula vya mafuta ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
Akizungumza na Mpanda Radio Fm kwa njia ya simu Mratibu wa Tiba manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Dk Gabriel Elias amesema kuwa magonjwa kama vile presha,shinikizo la damu,kisukari,saratani na magonjwa ya moyo yanaendelea kuwa changamoto ya afya duniani hivyo kufanya mazoezi ni njia mojawapo ya kuepukana na magonjwa hayo.
Aidha dk Elias amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kufanya mazoezi angalau ya kutembea ili kuboresha afya ya mwili ili kupunguza magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameainisha baadhi ya magonjwa yasiyoambukizwa kulingana na uelewa wao ambapo wameonekana kutokujua namna ya kuepukana na magonjwa hayo.
Kulingana na ripoti ya shirika la afya Duniani WHO,iliyochapishwa na the citizen,takriban watu billion 1.9 wanaugonjwa wa kisukari nchini ambapo shirika hilo limependekeza kufanya mazoezi ni njia bora ya kuimarisha afya na kudhibiti uzito.