Ubovu wa barabara kikwazo cha uchumi
10 January 2025, 12:14 pm
“Serikali kuchukua hatua za haraka za matengenezo ili kulifungua eneo hilo“
Na John Benjamin Katavi
Ubovu wa barabara inayounganisha kata ya Nsemulwa na Uwanja wa Ndege manispaa ya Mpanda mkoani Katavi ni kero ambayo inazorotesha ukuaji wa uchumi wa kata hizo licha ya serikali kutoa ahadi ya ujenzi wa barabara hiyo kupitia mradi wa Taktiki.
Wakizungumza na Mpanda Redio FM Wananchi wameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka za matengenezo ili kulifungua eneo hilo ambalo waendesha bajaji wamekuwa wakisita kuwapeleka abiria pamoja na kuwaongezea nauli.
Kutokana na malalamiko hayo, mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli ameeleza kuwa kinachosubiliwa kwa sasa ni kuanza ujenzi wa barabara hiyo.
Barabara hiyo ambayo Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango alipofika kufungua kituo cha Afya kata ya Nsemulwa aliuagiza uongozi wa mkoa kuhakikisha wanaijenga kwa haraka njia hiyo kwa kiwango cha lami.