Mpanda FM

Chatu azua hofu kwa wananchi mtaa wa Kasimba

9 January 2025, 1:17 pm

Katika picha maeneo mbalimbali ya mtaa wa Kasimba , wananchi, mwenyekiti wa mtaa na mfano wa picha ya nyoka aina ya chatu

Hofu imetanda miongoni mwao kwani huenda chatu huyo akaleta madhara kwa binadamu.

Na Lilian Vicent -Katavi

Wananchi wa mtaa wa Kasimba Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia uwepo wa nyoka aina ya chatu ambaye amekuwa tishio kwa kula mifugo kama vile kuku,bata na  mbuzi .

Wakizungumza na Mpanda Redio FM wananchi hao wamesema hali hiyo imepelekea hofu miongoni mwao kwani huenda chatu huyo akaleta madhara kwa binadamu.

Sauti za wananchi wakizungumzia matukio mbalimbali yanayotokea yakihusisha chatu hiyo.

Benard Elias Nswima mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba  amekiri kupokea taarifa kwa wananchi na ameshapeleka taarifa kituo cha polisi pamoja na kuwajulisha askari wa wanyama pori kwa hatua zaidi.

Sauti ya Benard Elias Nswima mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba

Sanjari na hayo Nswima amebainisha kuwa wamepanga kupita na vipaza sauti katika maeneo ya mtaa huo ili kuwajulisha wananchi juu ya uwepo wa hatari hiyo.

Sauti ya Benard Elias Nswima mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba