Mpanda FM

Mtoto wa miaka 8 afariki kwa kujinyonga, sababu kukosa nguo za sikukuu

3 January 2025, 10:05 pm

Kamanda wa jeshi la polisi Katavi .picha na Leah Kamala

wazazi hakikisheni mnatunza fedha kwa ajili ya kuwanunulia watoto nguo za sikukuu ili kuwaepushia watoto msongo wa mawazo

Mtoto mwenye umri wa miaka 8 amefariki dunia mkoani Katavi mara baada ya kujinyonga kutokana na kukosa nguo za sikukuu

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amesema mtoto huyo wa darasa la tatu amechukua uamuzi wa kujinyonga kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao baada ya kukosa nguo za sikukuu

Sauti ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani akizungumza

Kamanda Ngonyani amewashauri wazazi na walezi kujitahidi kuhifadhi fedha mapema kabla ya sikukuu hazijafika ili waweze kumudu kuwanunulia watoto wao nguo ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza ikiwemo msongo wa mawazo kwa watoto unaopelekea watoto kuchukua maamuzi yasiyofaa.