Waendesha bajaji Katavi watembelea wagonjwa, yatima
31 December 2024, 10:14 pm
“wameguswa kutoa msaada kwa watu hao wenye uhitaji kuliko kwenda kufanya starehe “
Na Samwel Mbugi-Katavi
Baadhi ya wanawake katika wodi ya wazazi pamoja na watoto yatima wanaoishi kituo cha mtakatifu Yohane Poul wa II Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametoa shukrani baada ya kupatiwa msaada wa vitu mbalimbali na umoja wa waendesha bajaji kwa kushirikiana na wadau .
Wakizungumza na Mpanda Radio fm wameshukuru kwa msaada huo ambapo wamewaomba wananchi na wadau wengine kuwa na moyo wakutoa kwa wahitaji.
Sauti za waliopatiwa msaada huo
Kwa upande wao wadau pamoja na umoja wa waendesha bajaji akiwemo mmoja ambaye ametumia siku hiyo kuadhimisha siku ya kuzaliwa wamesema kuwa wameguswa kutoa msaada kwa watu hao wenye uhitaji kuliko kwenda kufanya starehe .
Sauti za waendesha bajaji na wadau
Dr Richard Mshangila kutoka wodi ya wazazi manispaa ya Mpanda na Sista Eva Mkenyenge kutoka kituo cha mtakatifu Yohane Poul wa II wameshukuru kwa misaada iliyotolewa kwani ni njia mojawapo ya kuigusa jamii.
Sauti za Dr Richard Mshangila kutoka wodi ya wazazi manispaa ya Mpanda na Sista Eva Mkenyenge kutoka kituo cha mtakatifu Yohane Poul wa II
Miongoni mwa misaada iliyotolewa ni pamoja na bima ya afya kwa watoto wa tatu ,sukari ,sabuni. Soksi za watoto pamoja na juisi.