Meya Mpanda aiomba serikali msamaha wa matibabu vituo vya kulelea watoto yatima
26 December 2024, 6:33 pm
“Kutokana na kazi kubwa inayofanywa na walezi wa vituo vya kulelea watoto yatima kuna haja ya watoto hao kupata msamaha wa matibabu“
Na Edda Enock- Katavi
Mstahiki meya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi aiomba serikali kutoa msamaha wa matibabu kwa vituo vya kulelea watoto yatima
Haidary sumry ameyasema hayo alipotembelea kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo kata ya Nsemulwa December 25 mwaka huu.
Sauti ya mstahiki meya Manispaa ya Mpanda akizungumza
Sister.Rose Sungura ambae ni mlezi wa watoto yatima katika kituo hicho amemshukuru Mstahiki meya kwa kuwatembelea watoto hao na kuwapa faraja
Sauti ya Sister Rose Sungura akitoa shukrani
Nae Barnabas Chales ambae ni mmoja ya wananchi ambao waliongozana na mstahiki meya amewaomba wananchi kuwa na upendo na kuendelea kuwatembelea watoto hao.
Sauti ya mmoja ya wananchi waliohudhuria katika kuwapa faraja watoto hao
Mstahiki Meya ametembelea watoto hao December 25 mwaka huu akiwa na waandishi wa habari,viongozi mbalimbali na wananchi mkoani katavi.