

17 December 2024, 3:26 pm
“Makusanyo ya mwezi Julai hadi Novemba mwaka 2024,TRA imekusanya Sh. Bill 6.9“
Na John Mwasomola -Katavi
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoani Katavi imewataka wafanyabiashara ndani ya mkoa kuendelea kulipa kodi kwa hiari ili kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa Nchi.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya mamlaka hiyo kukusanya mapato na kufikia lengo kusudiwa.
Akizungumza katika Kikao ambacho kimefanyika december 17 2024katika , Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Katavi Nicolaus Migela amesema kutokana na makusanyo ya mwezi Julai hadi Novemba mamlaka imekusanya Sh. Bill 6.9.
Sauti ya Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Katavi Nicolaus Migela
Aidha amewataka wafanyabiashara wanapouza bidhaa zao watoe risiti kwa wateja, na wateja kudai risiti kwakua kwakutofanya hivyo ni njia moja wapo ya kukwepa kodi.
Sauti ya Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Katavi Nicolaus Migela
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara ambao wamehudhuria kikao hicho wametoa maoni yao na kuupongeza uongozi wa TRA Pamoja na kuomba kupatiwa elimu ya kutosha kwa wasio kua na uelewa na mapato.
Sauti ya wafanyabiashara ambao wamehudhuria kikao hicho
Akihitimisha kikao hicho meneja TRA Katavi Nicolaus Migela amesema watafanya kama walivyokubaliana katika kikao hicho na kuahidi ushirikiano wa Pamoja ili kuleta maslahi makubwa nchini na kutotegemea msaada nje ya nchi.