

16 December 2024, 12:48 pm
“Watumiaji wa vyombo vya moto wameahidi kufanyia kazi maelekezo waliopatiwa ili kujilinda“
Na John Benjamini -Katavi
Mkoa wa katavi umetajwa kuwa na takwimu chache za ajali barabarani kwa kipindi cha miezi sita kwa mwaka 2024.
Hayo yamebainishwa na kamishina wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani makao makuu Ramadhani Ng’anzi wakati akizungumza na madereva wa vyombo vya moto ambapo amewataka Watumiaji wa barabara mkoa wa Katavi kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha ajali
Sauti ya kamishina wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani makao makuu Ramadhani Ng’anzi
Kwa upande wao baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto wameahidi kufanyia kazi maelekezo waliopatiwa ili kujilinda na kutoa ushirikiano kwa baadhi ya madereva ambayo watavunja sheria na kanuni wanapokuwa bara barani na kupelekea kusababisha ajali.
Sauti ya watumiaji wa vyombo vya moto
Katika Hatua nyingine Ng’anzi amewataka watumiaji wa vyombo vya moto kuacha tabia ya kubeba idadi kubwa ya abiria kinyume sheria.