RC Katavi asikiliza kero za wafanyabiashara wamlalamikia kutolipwa madeni
4 December 2024, 8:19 pm
“halmashauri zimekuwa zikidaiwa madeni hayo kwa muda mrefu bila mafanikio“
Na Samwel Mbugi-Katavi
Wafanyabiashara mkoa wa Katavi wailalamikia serikali kutolipa madeni kwa wakati wanayodaiwa na baadhi ya wafanyabiashara ambao wanazidai halmashauri
Hayo yamesemwa na Aman Mahellah mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara katika kikao cha pili cha baraza la biashara Mkoa wa Katavi (RBC) ambapo amesema halmashauri zimekuwa zikidaiwa madeni hayo kwa muda mrefu bila mafanikio
Sauti ya Aman Mahellah mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, katika kikao hicho amezitaka halmashauri na Taasisi mbalimbali za Serikali zinazodaiwa na wafanyabiashara kulipa madeni ya Wazabuni na Watoa huduma mbalimbali katika halmashauri
Sauti ya mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
Hata hivyo mwanamvua amesema January 14, 2025 kutakuwa na kikao cha tathimini ya kuchunguza madeni yaliyopo katika halmashauri.