RC Katavi ahimiza haki katika uchaguzi wa serikali za mitaa
25 November 2024, 3:03 pm
“kila mwananchi aliyejiandikisha ana haki ya Kwenda kuchagua kiongozi anayemuona ataweza kumtumikia kwa miaka mitano.“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewahimiza wananchi wa mkoa wa Katavi waliojiandikisha katika daftari la mkazi kujitokeza kupiga kura November 27,2024 katika vituo walivyojiandikisha.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake November 25,2024 ambapo amesema kila mwananchi aliyejiandikisha ana haki ya Kwenda kuchagua kiongozi anayemuona ataweza kumtumikia kwa miaka mitano.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi
Mrindoko amewataka wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa Kutenda haki kwa vyama vyote vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo iliyowekwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Sauti ya mkuu wa mkoa akisisitiza wasimamizi kutenda haki
Hata hivyo Mrindoko amewahakikishia wananchi wote wa mkoa wa Katavi usalama katika kipindi chote cha kampeni na siku ya uchaguzi, ambapo amesema mkoa uko salama na wamejipanga vizuri katika kuhakikisha amani inatawala siku zote.