Katavi:wazazi,walezi watakiwa kulinda na kutetea haki za watoto
20 November 2024, 6:06 pm
Wazazi na walezi mkoani Katavi wametakiwa kulinda na kutetea haki za watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mpanda radio fm ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya watoto duniani inayo fanyika kila mwaka tarehe 20 wamebainisha kuwa malezi na misingi bora ya wazazi kwa watoto inasaidia watoto kutopata majanga yoyote.
sauti za wazazi na walezi
Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii manispaa ya Mpanda Anyulumiye Longo amebainisha haki za msingi za watoto kama vile haki ya kuishi ,haki ya kulindwa huku akibainisha kesi mbalimbali za matunzo kwa watoto pamoja na kezi za malezi kwa kutuoa elimu katika jamii kupitia njia mbalimbali ili kuweka usawa kwa watoto
afisa ustawi wa jamii manispaa ya mpanda Anyulumiye Longo
Nikodemas luhele ni mkurugenzi wa shirika la kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu( Tosovc) amebainisha malengo ya siku ya mtoto duniani ikiwa ni pamoja na kuhamasisha jamii kuzingatia mawazo na ndoto na mahitaji ya watoto katika maamuzi ya sasa ili kuleta mabadiliko chanya duniani.
Nikodemas luhele ni mkurugenzi wa shirika la kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu( Tosovc)
Maadhimisho ya siku ya watoto yamebebwa na kauli isemayo “ kusikiliza sauti za baadae” maadhimisho hayo yanahimiza kulinda haki za watoto .