Baadhi ya wananchi Katavi waeleza madhara ya kutopiga kura
18 November 2024, 2:58 pm
“Kutopiga kura kunaweza kusabababisha kuathiri maendeleo ya nchi na kupoteza nafasi ya kuchagua viongozi sahihi.“
Na Lear Kamala -Katavi
Zikiwa zimesalia siku chache kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa November 27 2024,baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni yao kuhusiana na madhara yanayoweza kujitokeza endapo hawatoshiriki kupiga kurakatika uchaguzi huo.
Wakizungumza na Mpanda Radio FM, wananchi hao wamesema kuwa kutopiga kura kunaweza kusabababisha kuathiri maendeleo ya nchi na kupoteza nafasi ya kuchagua viongozi sahihi.
Sauti ya baadhi ya wananchi wakieleza madhara ya kutopiga kura
Mkurugenzi wa asasi ya tuelimike kutoka Kijiji cha Isajandugu kata ya Nsimbo Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi Deoglas Mwaisaka amesema ikiwa idadi kubwa ya wananchi hawatoshiriki zoezi la kupiga kura matokeo ya uchaguzi yanaweza kuleta mashaka jambo litakalohatarisha misingi ya demokrasia.
Sauti ya mkurugenzi wa asasi ya tuelimike
Nae mratibu wa uchaguzi manispaa ya Mpanda Donald Pius ambaye amemwakilisha mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kuchagua viongozi watakaokuwa tayari kutatua changamoto zao katika jamii.
Sauti ya mratibu wa uchaguzi manispaa ya Mpanda Donald Pius
Wananchi wana haki ya kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuhakikisha kuwa viongozi wanachaguliwa kwa njia halali na yenye uwazi