Polisi Katavi wabaini wizi kwa abiria wasiopatiwa tiketi mtandao
21 October 2024, 11:23 am
SSP Deus Sokoni, Mwanasheria wa kikosi Cha usalama barabarani.picha na Anna Milanzi
“Kuna baadhi ya makondakta na mawakala ambao hawatoi tiketi mtandao kwa abiria na kuwapatia tiketi za mkono hali ambayo hupelekea abiria hao kuibiwa kwa kuongezewa nauli jambo ambalo ni kinyume na sheria.“
Na Anna Milanzi-Katavi
Katika kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua jeshi la polisi Kupitia kitengo Cha usalama barabarani Nchini limeendelea kutoa Elimu kwa madereva.
Akizungumza na madereva wa mabus yaendayo mikoani katika stand kuu ya Mkoa wa Katavi Mizengo Pinda alfajiri ya October 19 2024 ,mwanasheria wa kikosi Cha usalama barabarani SSP Deus Sokoni amewataka madereva kuzingatia Sheria za usalama barabarani ikiwemo kutozidisha abiria kwenye bus .
Sauti ya SSP Deus Sokoni, Mwanasheria wa kikosi Cha usalama barabarani
Sambamba na hilo amewataka Makondakta na ajent wa Bus hizo kuwapatia abiria tiketi mtandao huku akianisha kuwa Kuna baadhi ya Makondakta na ajent ambao hawatoi tiketi mtandao kwa abiria na kuwapatia tiketi za mkono hali ambayo upelekea abiria hao kuibiwa kwa kuongezewa nauli jambo ambalo ni kinyume na Sheria.
Sauti ya SSP Deus Sokoni, Mwanasheria wa kikosi Cha usalama barabarani
Ametoa wito kwao kuzingatia Sheria zote zinazopaswa kufuatwa na kueleza kwa atakae kiuka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yake