Wakulima Katavi wahitaji kupimiwa udongo katika mashamba yao
10 October 2024, 5:32 pm
“Baadhi yao wamekuwa wakilima kwa mazoea kwani hawatambui kuwa udongo unahitaji nini wakati wa kilimo”
Na Roda Elias -Katavi
Baadhi ya wakulima wa kijiji Kamsanga kata ya Mnyagala wilayani Tanganyika mkoani Katavi wameomba kupimwa kwa udongo wao mashambani kabla ya kuanza kilimo.
Wakulima hao wameainisha kuwa Miongoni mwao wamekuwa wakiweka mbolea awamu moja ama mbili licha ya elimu ya kilimo kuwataka kuweka mbolea shambani kwa awamu tatu.
Wakizungumza na Mpanda Radio FM wakulima hao wamesema kuwa elimu wanayopatiwa ina faida ingawa baadhi yao wamekuwa wakilima kwa mazoea kwani hawatambui kuwa udongo unahitaji nini wakati wa kilimo
Kwa upande wake afisa kilimo mkoa wa katavi amewataka wakulima ambao bado hawajafikiwa kupimiwa ardhi zao wawe wavumilivu kwani serikali injua nini cha kufanya .