Wananchi Katavi waomba watoto waishio mazingira hatarishi wasaidiwe
6 October 2024, 12:30 pm
picha na mtandao
“serikali itoe Elimu kwa wazazi kuhusiana na malezi bora kwa mtoto na kuwapa mikopo wazazi ili kuwasaidia kukidhi mahitaji madogo madogo kama vile kumpeleka mtoto shule,malazi na chakula ili Watoto waepukane na makundi hayo hatarishi.“
Na Edda Enock -Katavi
Baadhi ya Wananchi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuwasaidia Watoto ambao wanajiunga na makundi hatarishi na hatimae kujihusisha na uporaji na unyang’anyanyi.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa serikali itoe Elimu kwa wazazi kuhusiana na malezi bora kwa mtoto na kuwapa mikopo wazazi ili kuwasaidia kukidhi mahitaji madogo madogo kama vile kumpeleka mtoto shule,malazi na chakula ili Watoto waepukane na makundi hayo hatarishi.
Sauti ya wananchi wakizungumza
Hayo yanajiri kufuatia kauli ya Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko aliyoitoa September 28/2024 katika viwanja vya polisi Buzogwe ambapo alipiga marufuku Watoto kutokujihusisha na makundi hatarishi
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi akizungmza