Mpanda FM

Vikwazo vinavyokwamisha wanawake kuwania uongozi vyabainika Katavi

6 October 2024, 12:13 pm

Picha na mtandao

Vikwazo mbalimbali ikiwemo rushwa ya ngono na imani potofu vimekuwa ni mwiba kwao katika kugombea nafasi za uongozi.

Na Ben Gadau -Katavi

Baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Nsimbo mkoani Katavi wameelezea  vikwazo vinavyopelekea wanawake kutowania nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, Novemba 27, 2024.

Wakizungumza na Mpanda Radio FM, wananchi hao wamesema kuwa vikwazo mbalimbali ikiwemo rushwa ya ngono na imani potofu vimekuwa ni mwiba kwao katika kugombea nafasi za uongozi.

Sauti za wananchi wakizungumza

Miongoni mwa sababu zinazowadhoofisha wanawake wengi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi zimeelezewa na Douglas Mwaisaka ambaye ni mkurugenzi asasi ya Tuelimike kutoka kijiji cha Isajandugu kata ya Nsimbo, halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi

Sauti ya Douglas Mwaisaka Mkurugenzi asasi ya Tuelimike

Katika kuhakikisha ushiriki wa wanawake unaongezeka, wanawake wenye ndoto za kugombea uongozi wameshauriwa kuanza kujifunza kutoka kwa wanawake wanasiasa waliowatangulia ili kuongeza ujasiri na uthubutu wa kukabiliana na vikwazo kuelekea kwenye uchaguzi.