Mpanda FM

RC Katavi awataka viongozi wa mitaa, kata kutoa elimu ya uchaguzi

20 September 2024, 10:54 am

Mkuu wa mkoa wa Katavi .picha kutoka maktaba

” Wamepokea Maelekezo Ya Mkuu Wa Mkoa Na Tayari Wameshaanza Kutoa Elimu Kwa Maeneo Mbalimbali

Na Leah Kamala-Katavi

Mkuu Wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka watendaji  wa serikali Katika mitaa, vitongoji na vijiji kutoa elimu kwa wananchi juu ya zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika novemba  27 2024.

Mrindoko ametoa maagizo hayo katika kikao kazi na watendaji  kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa uliopo mjini Mpanda sambamba na kusikiliza kero kutoka kwa watendaji.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi akizungumza

Kwa upande wao washiriki waliohudhuria kikao kazi hicho akiwepo mtendaji wa kata ya Mamba Peter Mseruka Na mtendaji wa kijiji cha Kabunde wamesema kuwa wamepokea maelekezo ya mkuu wa mkoa na tayari wameshaanza kutoa elimu kwa maeneo mbalimbali

Sauti za watendaji

Mrindoko amewasisitiza  wananchi juu ya utunzaji wa mazingira na kusema kuwa mkoa wa Katavi ni kinara katika biashara ya hewa ukaa hivyo amewahimiza kutunza na kulinda misitu pamoja na vyanzo vya maji kwa matumizi ya baadae.