Katavi: 97 mbaroni kwa tuhuma za uhalifu
6 September 2024, 1:11 pm
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Katavi ACP David Mutasya akionyesha vitu mbalimbali walivyokutwa navyo watuhumiwa .picha na Roda Elias
“Jeshi la polisi limetoa muda kwa wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha sulaha hizo katika vituo vya polisi au ofisi za serikali“
Na Roda Elias -Katavi
Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata watuhumia 97, wanaojihusisha na vitendo vya kiuhalifu huku wakiwa na vielelezo mbali mbali.
Kaimu kamanda wa polisi ACP DAVID MUTASYA ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu hali ya ulinzi na usalama mkoani Katavi kupitia doria, misako na kesi za mahakamani kwa kipindi cha mwezi Agost.
Sauti ya Kaimu kamanda wa polisi ACP David Mutasya akizungumza
Aidha ACP Mutasya ametoa wito kwa wananchi kuishi kwa kufuata taratibu na sheria ili kuwaibua na kuwafichua wahalifu lakini pia kulinda mali na rasilimali za taifa .
Sauti ya kaimu Kamanda akitoa wito
Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa kwa sasa wanaishi kwa amani na utulivu kwani uhalifu umepungua na kupongeza jeshi la polisi kutokana na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama mkoani hapa .
Sauti za wananchi wakitoa maoni yao
Sanjari na hayo jeshi la polisi limetoa muda kwa wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha silaha hizo katika vituo vya polisi au ofisi za serikali, huku zoezi hilo likiwa limeanza l tarehe 1/9/2024 na linatarajiwa kumalizika 30/9/2024 .