Mpanda FM

Wananchi Katavi wasisitizwa kuwa wazalendo

4 September 2024, 9:32 am

katika picha waliokaa upande wa kushoto ni mwenyekiti wa taasisi zisizo za kiserikali katavi ,anayefuatia ni katibu tawala mkoa wa katavi na kulia ni afisa maendeleo mkoa wa katavi.picha na Rachel Ezekia.

“lengo kuu la kukuza uzalendo ni kulinda rasilimali za nchi,kutunza siri za nchi na kutetea taifa letu.

Na Rachel Ezekia- Katavi

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuwa wazalendo ili kufikia azma ya kujenga taifa lenye mshikamano.

 Wito huo umetolewa na Anna Shumbi afisa maendeleo mkoa  wa Katavi katika mkutano wa jukwaa la mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa wa Katavi  ambapo amesema matokeo ya kuwa na uzalendo ni kuwepo kwa jamii inayowajibika kwa kujitolea na kufanya kazi kwa bidii ,kukuza Uchumi wa nchi kuleta mageuzi ya kifikra na mitazamo Chanya katika jamii.

 Sauti ya Anna Shumbi Afisa maendeleo mkoa  wa Katavi akizungumza

Shumbi Ametaja walengwa katika kukuza moyo wa uzalendo  ni Pamoja na wana siasa,wafanyabiashara wazazi na walezi watu mashuhuri katika jamii Watoto na vijana viongozi wa asasi za kiraia huku  lengo kuu la kukuza uzalendo ni kulinda rasilimali za nchi,kutunza siri za nchi na kutetea taifa .

Sauti ya Anna Shumbi akizungumza

Kwa upande wananchi mkoani hapa  wamebainisha kuwa jamii inatakiwa kuwa na umoja ili kuwa na uzalendo .

Sauti za wananchi wakizungumza

Sambamba na hilo wamesema jamii inapaswa kukemea vitendo ambavyo vimekuwa vikididimiza uzalendo baina yao.