Mpanda FM

Wawili mbaroni tuhuma za mauaji Katavi

13 August 2024, 8:03 pm

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani

“Watuhumiwa hao wawili ni Japheth Didas miaka 32 na Shabani Maelezo miaka 64 ambao ni wakazi wa mkoa wa Rukwa.”

Na Lear Kamala -Katavi

Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya dereva bodaboda yaliotokea Julai 24 mkoani Katavi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amesema watuhumiwa hao baada ya kutekeleza mauaji walichukua pikipiki ya marehemu na kutokomea kusikojulikana.

Baada ya Jeshi la Polisi kupokea taarifa hizo lilianza msako mkali na hatimaye kuzaa matunda kwa kuwakamata watuhumiwa na kuonyesha walipouzia pikipiki hiyo.

Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi

Kwa upande wao baadhi ya madereva bodaboda Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesema wizi wa pikipiki umekua kero kwao huku wakilishukuru Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.

Sauti ya baadhi ya madereva bodaboda Manispaa ya Mpanda wakizungumza

Kamanda Ngonyani amesema watuhumiwa hao bado wanaendelea kuhojiwa ili kubaini mtandao mzima wa wizi wa pikipiki katika mkoa wa Katavi na mara baada ya mahojiano watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.