Katavi: Vijana watakiwa kuchangamkia fursa katika sekta ya kilimo
24 July 2024, 12:00 pm
Wajumbe wa kikao cha jukwaa la vijana la kilimo katika ukumbi wa LATCU uliopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.picha na Lilian Vicent
“wajumbe walioshiriki wamebainisha kuwa kupitia jukwaa hilo wanatarajia vijana wataendea kuhamasika“
Naa Lilian Vicent Katavi
Vijana mkoani Katavi wameshauriwa kutumia sekta ya kilimo kama fursa kupitia majukwaa ya kilimo .
Rai hiyo imetolewa na Faridu Mtiru Afisa kilimo mkoa wa katavi kwenye kikao cha jukwaa la vijana la kilimo katika ukumbi wa LATCU uliopo manispaa ya Mpanda mkoani hapa .
Sauti ya Faridu Mtiru Afisa kilimo mkoa wa katavi
Katika hatua nyingine Mtiru amesema kuwa vijana walioshiriki katika kikao hicho wanajihusisha na sekta ya kilimo hivyo watasaidia kuondoa mitazamo hasi iliyopo kwa baadhi ya vijana kuhusiana na sekta ya kilimo.
Sauti ya Faridu Mtiru Afisa kilimo mkoa wa katavi
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya mlele pamoja na baadhi ya wajumbe walioshiriki wamebainisha kuwa kupitia jukwaa hilo wanatarajia vijana wataendea kuhamasika kuingia kwenye sekta ya kilimo.
Sauti ya Afisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya wilaya ya mlele pamoja na baadhi ya wajumbe walioshiriki
Kikao hicho cha jukwaa la vijana la kilimo kimehudhuriwa na wajumbe ambao ni vijana wanaojihushisha na sekta ya kilimo, maafisa kilimo pamoja na maafisa maendeleo kutoka halmashauri mbalimbali..