Mpanda FM

Bodaboda Katavi wamkataa mwenyekiti wao, wamtaka ajiuzulu

20 July 2024, 5:41 pm

Baadhi ya madereva bodaboda waliojitokeza katika kikao hicho.picha na John Mwasomola

“Wamemtaka kiongozi huyo kuachia nafasi yake ya uenyekiti ili kupisha uchunguzi kutokana na shutuma za upotevu wa pesa taslimu kiasi cha laki 6 na thelathini.

Na Ben Gadau -Katavi

Baadhi ya maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda Mkoani Katavi wamemtaka mwenyekiti wa chama chao Isack Daniel Joseph kujiudhuru nafasi yake ili kupisha uchunguzi wa shutuma zinazo mkabili.

Wamezungumza hayo katika kikao kilicho fanyika katika ukumbi wa police club ambapo wamemtaka kiongozi huyo kuachia nafasi yake ya uenyekiti ili kupisha uchunguzi kutokana na shutuma za upotevu wa pesa taslimu kiasi cha laki 6 na thelathini.

Sauti za Madereva bodaboda wakizungumzia suala hilo

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa chama cha maafisa usafirishaji Mkoa wa Katavi Maiko Kamande amesema kuwa tayari pesa hizo zimerejeshwa katika uongozi wa chama hicho huku akiwataka madereva hao kuendelea kushikamana katika kipindi.

Sauti ya Kaimu Mwenyekiti wa chama cha maafisa usafirishaji Mkoa wa Katavi Maiko Kamande

 Aidha akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Mwenyekiti huyo wa bodaboda Mkoa ISACK DANIEL JOSEPH ambaye anatajwa kwenye upotevu wa pesa hizo zilizo rejeshwa katika kikao hicho amewataka madereva bodaboda kuendelea kuwa watulivu huku akisema hivi karibuni anatarsjia kuwa na kikao ambacho kitatua muafaka wa jambo hilo.

Sauti ya Mwenyekiti wa bodaboda ISACK DANIEL JOSEPH akizungumza

Wakwanza kutoka kushoto ni kaimu makamu mwenyekiti bodaboda Mkoa,wa pili kutoka kushoto mwenyekiti bodaboda mkoa wa katavi watatu kutoka kushoto ni mwenyekiti bodaboda wilaya ya Mpanda wanne kutoka Kushoto na wa mwisho ni katibu na katibu msaidizi bodaboda mkoa wa Katavi