Bilioni 67 kuinua uchumi wa mkulima wa tumbaku Katavi
19 July 2024, 12:00 am
Zao la tumbaku likiwa shambani. Picha na mtandao
“Uzalishaji wa zao hilo umepanda kutoka kilo milioni 6 hadi kilo milioni 11 ambapo ongezeko hilo limesababishwa na serikali nchini Tanzania kuongeza kampuni 11 kununua zao hilo.“
Na John Benjamini -Katavi
Zaidi ya shilingi bilioni 67 zimepatikana kwa wakulima wa zao la tumbaku katika mkoa wa Katavi kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2023/2024.
Mkurungezi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Stanley Mnovya amesema kwa msimu 2023/2024 mkoa wa Katavi uzalishaji wa zao hilo umepanda kutoka kilo milioni 6 hadi kilo milioni 11 ambapo ongezeko hilo limesababishwa na serikali nchini Tanzania kuongeza kampuni 11 kununua zao hilo.
Sauti ya Mkurungezi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania
Kwa upande wa wakulima wa tumbaku mkoani Katavi wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassani kwa kupambana kutafuta masoko ya uhakika na kusimamia ulipwaji wa fedha zao kwa wakati tofauti na misimu mingine.
Sauti ya wakulima wa tumbaku mkoani Katavi
Katika hatua nyingine Mnovya amesema katika mapato yaliyopatikana kwa wakulima yameweza kunufaisha halmashauri zote zinazolima zao hilo ambapo zaidi ya kiasi cha shilingi bilion 2 kama ushuru zimepatikana.