Katavi: Rais Samia awataka wazazi na walezi kuwaacha watoto wasome
16 July 2024, 11:50 am
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan.picha na Samwel Mbugi
“Rais Samia ameyasema hayo mara baada ya kutembelea hospitali ya rufaa ya mkoa na kujionea hali ilivyo ya watoto walio na umri chini ya miaka 18 kujifungua watoto “
Na Samwel Mbugi -Katavi
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi kuwaacha watoto wasome ili watimize ndoto zao pia kuwaepusha mimba za utotoni.
Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi baada ya kutembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi kuwa angalau mtoto anaejifungua awe na umri wa kuanzia miaka 19 na kuendelea.
Sauti ya Rais Samia akizungumza na wananchi
Aidha katika hatua nyingine amewataka wakazi wa mkoa wa Katavi kujiunga na bima ya afya ambayo itasaidia kutibiwa na familia yako bila shida yoyote pindi utakapokuwa na changamoto ya kupatwa na ugonjwa.
Sauti ya Rais Samia akizungumza na wananchi
Hata hivyo Rais Samia ameupongeza mkoa wa Katavi kwa kazi kubwa ya maendeleo yanayofanyika na mganga mkuu wa hospital ya rufaa kwa kazi zuri wanayoifanya ya kutunza hospital pamoja na huduma zinazotolewa hapo na watumishi.