Kutoeleweka dhana ya 50 kwa 50 chanzo cha malezi ya mzazi mmoja mkoani Katavi
16 July 2024, 9:43 am
Picha na Mtandao
“malezi ya mzazi mmoja na Wamekuwa wakitoa elimu katika jamiii ili Watoto wapate malezi ya wazazi pande zote.“
Na Rachel Ezekia-Katavi
Kufuatia takwimu za zinazoonesha ongeza la Watoto wanaolelewa na mzazi mmoja, Wazazi na walezi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha wanawalea Watoto katika misingi bora ya malezi.
Akizungumza na Mpanda Redio Fm Afisa ustawi wa jamii Thabiti Mlagano amebainisha kuwa dhana ya uelewa duni ya 50 kwa 50 inapelekea ongezeko la malezi ya mzazi mmoja katika jamii huku akiwataka wazazi na walezi kuiilewa dhana hiyo ili isiathiri malezi ya Watoto.
Sauti ya Afisa ustawi wa jamii Thabiti Mlagano
Aidha ameongeza kuwa takwimu zinaonesha kuwa manispaa ya Mpanda kumekuwa na kesi za malezi ya mzazi mmoja na Wamekuwa wakitoa elimu katika jamiii ili Watoto wapate malezi ya wazazi pande zote.
Sauti ya afisa ustawi manispaa
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa hali ya kipato na wanaume kudharaulika inapelekea wanawake kuwalea Watoto kwa nguvu zao wenyewe huku wakiamini kuwa malezi bila baba yanawezekana.