Wananchi Katavi wamshukuru Rais Samia kwa kuboresha Miundombinu ya afya
16 July 2024, 9:09 am
Wananchi ambao wamejitokeza kumsikiliza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake mkoani humo
“awali walikua hawapati huduma ambazo zinapatikana katika hospitali hiyo kwa sasa.“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Wananchi mkoani Katavi wamemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano Wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya afya.
Wakizungumza baadhi ya wananchi waliopata nafasi ya kupata huduma katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Katavi wamesema kuwa awali walikua hawapati huduma ambazo zinapatikana katika hospitali hiyo kwa sasa.
Sauti za wananchi waliopata nafasi ya kupata huduma katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Katavi
Madaktari na wataalam wa Hospitali hiyo wamepongeza jitihada za Serikali kuboresha huduma muhimu na kuendelea kuwajengea uwezo madaktari wa kuwahudumia wananchi kupitia mafunzo.
Sauti za madaktari wamepongeza jitihada za serikali
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Katavi ambapo amekemea suala la mimba za utotoni na kuitaka jamii kuacha kuozesha watoto waliochini ya umri wa miaka 20.
Sauti ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania