Katavi :Uzinduzi wa wiki ya jumuiya ya wazazi jamii yaaswa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili
8 July 2024, 9:37 pm
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman
jumuiya hiyo imekuwa msingi wa kutoa viongozi Bora ambao Wana maadili na wenye uwezo wa kuwatumikia Wananchi Kwa Ufanisi.
Na Samwel Mbugi -Katavi
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman ametoa wito Kwa wazazi kuendelea kuhimiza malezi na kudumisha Mila na desturi za kitanzania ili kukabiliana na janga la mmomonyoko wa maadili ambao umeendelea kuwaathiri vijana Kwa kujiiingiza kwenye makundi yasiyofaa kama vile Matumizi ya madawa ya kulevya.
Ameyasema hayo Katika sherehe za Uzinduzi wa wiki ya wazazi kitaifa iliyofanyika Katika Wilaya ya mlele Ambayo yatahitimishwa siku ya tarehe 13 katika viwanja vya shule ya msingi kashaulili manispaa ya Mpanda mkoa wa katavi.
Ameongeza kuwa serikali ya Tanzania na serikali ya Zanzibar zinathamini na kufarijika na umoja wa wazazi kwa kusimamia sekta ya elimu na tamaduni za watanzania
Sauti ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman
Amesema Jumuiya ya wazazi wanao wajibu kuendelea kuhimiza malezi, kwani jumuiya hiyo imekuwa msingi wa kutoa viongozi Bora ambao Wana maadili na wenye uwezo wa kuwatumikia Wananchi Kwa Ufanisi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hozza Mrindoko ameishukuru jumuia ya wazazi na chama cha mapinduzi CCM kwa kuteua mkoa wa Katavi kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo kitaifa.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm mkoa wa Katavi Iddy Kimanta ametoa pongeza kwa wabunge wote wa mkoa wa Katavi kwa ushirikiano wanaouonyesha katika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm mkoa wa Katavi Iddy Kimanta
Hata hivyo Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda amesisitiza kuwepo kwa umoja na mshikamano ambao unasaidia kudumisha amani na utulivu kwa watanzania wote.
Sauti ya Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda
Maadhimisho ya wiki ya wazazi Kwa chama Cha Mapinduzi CCM yanafanyika mkoani Katavi kitaifa, na kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni ushindi wa chama Cha Mapinduzi (CCM) 2024/2025 jumuiya ya wazazi tupo mstari wa mbele