Mpanda FM

Watuhumiwa 12 wa mauaji washikiliwa na jeshi la polisi Katavi

8 July 2024, 12:37 pm

Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.Picha na Rachel Ezekia

Watuhumiwa wengine wamekamatwa kwa makosa mbalimbali ya silaha haramu aina ya gobore madawa ya kulevya,pamoja na  pombe ya moshi.

Na Rachel Ezekia -Katavi

Jeshi la polisi mkoa wa katavi linawashikilia watuhumiwa 12 wakijihusisha katika matukio ya mauaji ambayo yametokea kwa nyakati  tofauti mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi SACP Kaster  Ngonyani ametoa taarifa hiyo akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa watuhumiwa wengine wamekamatwa kwa makosa mbalimbali ya silaha haramu aina ya gobore madawa ya kulevya,pamoja na  pombe ya moshi.

Sauti ya Kamanda wa jeshi la Polisi SACP Kaster Ngonyani

Aidha amebainisha jumla ya watuhumiwa 21 wamefikishwa mahakamani na kuhukumiwa vifungo mbalimbali ikiwepo watuhumiwa 5 kuhukumiwa kifungo cha miezi 12 kwa kosa la kupatikana na mazao ya misitu pamoja na kuingia ndani ya hifadhi bila kibali.

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Katavi

Katika hatua nyingine amesema kuwa jeshi la polisi kitengo cha polisi jamii dawati la jinsia na watoto na wakaguzi kata ambao wapo katika kila kata wamefanikiwa kutoa elimu kwa umma kupitia mikutano ya hadhara vipindi vya redio na kuitaka jamii kuachana na vitendo vya kihalifu.