Mpanda FM

Maadhimisho ya jumuiya ya wazazi Katavi, wananchi watakiwa kutumia fursa

8 July 2024, 11:44 am

Menyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Katavi Iddi Kimanta akiwa katika kiti cha mbele akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya siasa ya mkoa

Maadhimisho hayo yatafunguliwa julai 8 Inyonga wilayani Mlele

Na Betord Chove-Katavi

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kutumia fursa kukuza biashara kufuatia maadhimisho ya jumuiya wa wazazi ya chama Cha Mapinduzi (CCM ) Taifa.

Akizungumza na waandishi wa Habari mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi ccm mkoa wa Katavi Iddi Kimanta amesema maadhimisho hayo yatafunguliwa julai 8 Inyonga wilayani Mlele ambapo yatafunguliwa na makamu mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Ccm Zanzibar na Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar dk Hussein Ally Mwinyi na kufungwa julai 13 na mwenyekiti wa ccm bara na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Bara dk Samia Suluhu Hassan wilayani Mpanda mkoani hapa.

Sauti ya Iddi Kimanta mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Katavi

Aidha Kimanta amesema katika wiki hiyo kutakuwa na shughuli mbalimbali zitazoambatana na maadhimisho hayo na kuwataka wananchi kutumia fursa ya kuwepo Kwa maadhimisho hayo mkoani hapa.

 Sauti ya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Katavi Iddi Kimanta

Maadhimisho ya wiki ya wazazi chama Cha Mapinduzi Taifa yanafanyika mkoani Katavi na kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni ushindi wa chama Cha Mapinduzi (ccm) 2024/2025 jumuiya ya wazazi tupo mstari wa mbele.