TIRA yasisitiza wananchi Katavi kujiunga na bima
2 July 2024, 6:56 pm
Kamishna wa Bima Tanzania TIRA Bagayo Saqwale mwenye tai pamoja na RC Katavi Mwanamvua Mrindoko wanne kutoka kushoto katika picha ya pamoja na viongozi wengine. Picha na Ben Gadau
“Kutumia bima kuna faida yanapotokea majanga huku akisema wanatarajia kusogeza huduma kwa wananchi wa mkoa wa Katavi“
Na Ben Gadau Katavi
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA wameiasa jamii mkoani Katavi kuendelea kutumia huduma ya bima ili kujikinga na madhara pindi yanapotokea.
Akizungumza kamishna wa Bima Tanzania Bagayo Saqwale amesema kutumia bima kuna faida yanapotokea majanga huku akisema wanatarajia kusogeza huduma kwa wananchi wa mkoa wa Katavi ambapo awali walilazimika kwenda mikoa ya magharibi kupata huduma hiyo.
Kurenje Mbura ni Meneja wa TIRA Kanda ya ziwa Tanganyika amesema kwa sasa wanaendelea kutoa elimu ya umuhimu wa kutumia bima sambamba na kusajili makampuni na wafanyabiashara ambao wanahitaji kufanya biashara ya bima.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amepongeza jambo hilo huku akiwaasa wananchi mkoani Hapa kujitokeza kupata elimu na kutumia bima zitakazo wasaidia pindi yanapotokea madhara.