Mpanda FM

Mtoto mwenye umri wa miaka 8 alawitiwa Katavi

18 June 2024, 5:52 pm

Picha na mtandao

Tukio kama hili ni la nne kutokea katika kitongoji hicho

Na Samwel Mbugi- Katavi

Mtoto mwenye umri wa miaka 8 ambaye jina lake limehifadhiwa kutoka kijiji cha Dirifu Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi inadaiwa kalawitiwa na kijana aliyejulikana kwa jina moja la Shingisha.

Akizungumza na Mpanda Radio Fm Mlezi wa mtoto huyo ambae ni babu yake,  jina lake limehifadhiwa, amesema kuwa baada ya kupata taarifa hizo amefanya jitihada za kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha polisi,hospital ili kupata matibabu na hatua nyingine za kisheria.

Sauti ya mlezi wa mtoto huyo akielezea tukio lilivyokuwa

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Msangama Kijiji cha Dirifu Regna Josephat Salia amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza ni  tukio la nne kutokea katika kitongoji hicho.

Sauti ya mwenyekiti wa kitongoji cha Msangama akizungumzia tukio hilo na hali halisi ya matukio ya namna hiyo

Nae Tabibu wa Magonjwa ya inje (OPD) kutoka Hospital ya Manispaa ya Mapanda mkoa wa Katavi Godfrey Bartazali amethibitisha kupokea Mtoto huyo na kumfanyia vipimo ambavyo vilithibitisha kuwa amefanyiwa ukatili huo.

Sauti ya Tabibu wa Magonjwa ya inje (OPD) kutoka hospitali ya manispaa ya Mapanda mkoa wa Katavi Godfrey Bartazali akithibitisha tukio hilo

Mpanda Radio Fm inaendelea kumtafuta kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi kwa ajili ya ufafanuzi zaidi wa tukio hilo.