Mpanda FM

Madereva Tax Katavi watakiwa kufuata sheria za usalama barabarani

12 June 2024, 3:17 pm

mkaguzi msaidizi Jofrey Brighton kutoka jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani mkoani Katavi akiwa anafanya ukaguzi

baadhi ya madereva wamekuwa wakifanya makosa ya kuzidisha abiria, kupakia abiria pamoja na mizigo hatarishi

Na John Benjamini-Katavi

Madereva wa Tax maarufu probox halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ikiwemo kutozidisha abiria.

Hayo yamezungumzwa na mkaguzi msaidizi Jofrey Brighton kutoka jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani ambapo ameleeza kuwa kuna baadhi ya madereva wamekuwa wakifanya makosa ya kuzidisha abiria, kupakia abiria pamoja na mizigo hatarishi hali ambayo ni hatari kwa abiria na watumiaji wengine wa barabara.

Sauti ya mkaguzi msaidizi Jofrey Brighton kutoka jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani

Kasanga Alubano Ni mwenyekiti wa madereva amekiri kuwepo kwa baadhi ya madereva wanaofanya vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria za usalama barabarani na kuwasihi madereva kufuata taratibu na sheria ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.

Sauti ya mwenyekiti wa madereva amekiri kuwepo kwa baadhi ya madereva wasiozingatia sheria wakiwa barabarani

Kwa upande wao baadhi ya madereva hao wamesema baadhi ya madereva wamekuwa wakiingiwa na tamaa ya fedha hali ambayo inapelekea kubeba abiria zaidi kinyume na uwezo wa gari na kuliomba jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kuwachukulia hatua madereva ambao hawazingatii sheria za usalama za barabarani.

Sauti ya madereva wakieleza namna ambavyo baadhi yao wanakiuka sheria za usalama barabarani