Mpanda FM

Katavi,Wanafunzi watatu wanywa kemikali wakiwa maabara mmoja kati yao afariki

3 June 2024, 12:28 pm

Wananchi pamoja na wanafunzi waliojitokeza katika mazishi ya mwanafunzi huyo.picha na millard ayo

Wanafunzi watatu,  wawili wasichana na mmoja wa kiume  Kutoka katika shule ya st Merrys iliyopo manispaa ya Mpanda  huku mwanafunzi huyo wa kiume akipatiwa rufaa ya Kwenda kutibiwa katika hospitali ya bugando ambako alifariki dunia.

Na Rachel Ezekia-Katavi

Mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari st.Marry’s iliyopo manispaa ya Mpanda Luis Emmanuel (17) amefariki baada ya kunywa kemikali inayodhiniwa kuwa ethanol katika maabara ya shule hiyo akiwa na wanafunzi wengine wawili.

Akizungumza na Mpanda radio fm Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi Dk serafine Patrice amekiri kuwapokea wanafunzi watatu  wawili wasichana na mmoja wa kiume  Kutoka katika shule ya st Merrys iliyopo manispaa ya Mpanda  huku mwanafunzi huyo wa kiume akipatiwa rufaa ya Kwenda kutibiwa katika hospitali ya bugando ambako alifariki dunia.

Sauti ya Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi Dk Serafine Patrice

Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi  SACP Kaster Ngonyani Amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Wanafunzi hao watatu ni wa kidato cha nne katika shule hiyo walikuwa wakifanya usafi katika maabara ya kujifunzia masomo ya sayansi kwa vitendo iliyopo shuleni hapo huku wakisimamiwa na mwalimu John Mtafya ambaye alitoka nje kuendelea na shughuli nyingine za kimasomo .

Sauti ya Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi  SACP Kaster Ngonyani akithibitisha kutokea kwa tukio hilo

 Wanafunzi wengine Evangelist Deodatus (20) mpaka sasa anaendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi na Anastasia Zakayo (17) hali yake ni njema na anaendelea na masomo.