Mpanda FM

Waziri Jafo :Katavi tunzeni mazingira

30 May 2024, 1:43 pm

picha na Site tv

uharibifu wa mazingira unaleta athari hasa ya mabadiliko ya tabianchi jamii inapaswa kuyatunza mazingira

Na Betord Chove -Katavi

Waziri wa Nchi (Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Saidi Jafo Amewaagiza wakuu wa Mikoa nchini  kutekeleza mpango wa kuhamia kwenye nishati safi ya kupikia.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi  Wa wiki ya Mazingira ambapo amewaomba Watanzania kutumia nishati safi ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi zinazotokana na uharibifu wa mazingira

Sauti ya waziri wa nchi (muungano na mzingira, Dkt.Selemani Saidi Jafo akisisitiza matumizi ya nishati mbadala

Aidha Waziri Jaffo amewataka wananchi kuacha kuharibu mazingira na kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya mkoa katika kupanda miti.

Sauti ya waziri wa Nchi (Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Saidi Jafo akisisitiza matumizi ya nishati mbadala

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameishukuru Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuleta uzinduzi wa wiki ya mazingira mkoani hapa na kumhakikishia waziri kuendelea kutunza mazingira na kuhakikisha taasisi zinahamia kwenye matumizi ya nishati safi.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza na kutoa shukrani na kuhakikisha utunzaji wa mazingira unasimamiwa

Ufunguzi wa wiki ya Mazingira yamefanyika mkoani Katavi katika halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele na maadhimisho hayo yataambatana na kauli mbiu isemayo  urejeshwaji wa ardhi, ustahimilivu wa hali ya Jangwa na ukame.