Mpanda FM

Wananchi kumlinda binti mwenye ulemavu dhidi ya mimba za utotoni

30 May 2024, 12:03 pm

Viti mwendo sambamba na nyenzo zingine za kusaidia watu wenye ulemavu kutoka sehemu moja kwenda nyingine .picha na Mtandao

wasichana wenye ulemavu wana ndoto na wanapaswa kufikia malengo yao ,jamii inapaswa kuwalinda wasichana wenye ulemavu

Na Ben Gadau- Katavi

Wazazi na walezi manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kushirikiana kumlinda msichana mwenye ulemavu dhidi ya mimba za utotoni.

Wito huo umetolewa na afisa ustawi wa jamii manispaa ya Mpanda Anilume Longo ambapo amesema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi  kushiriki  kumlinda msichana mwenye ulemavu dhidi ya mimba za utotoni huku akitaja mila na desturi kuwa  moja ya sababu inayopelekea kuongezeka kwa mimba za utotoni.

Sauti ya afisa ustawi wa Jamii manispaa ya Mpanda Anilume Longo

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wametoa maoni mseto huku wakiendelea kutoa wito kushirikiana katika kumlinda msichana mwenye ulemavu dhidi ya mimba za utotoni.

Sauti za wananchi wakitoa maoni yao juu ya kumlinda msichana mwenye ulemavu

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto iliyosomwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Oct 28/ 2023, imeonesha Kuongezeka kwa viwango vya mimba za utotoni katika baadhi ya mikoa(Songwe 45%, Ruvuma 32%, Katavi 34%, Mara 31%, Rukwa 30%, Njombe 25.5%, Dar Es Salaam 11%-18%.