Misitu 30 kuboresha biashara ya Kaboni Katavi
30 May 2024, 10:36 am
Mkuu wa mkoa wa Katavi akiwa wilayani Tanganyika .picha na site tv
“Halmashauri zote mkoani katavi zinapaswa kutunza mazingira ili kunufaika na biashara ya hewa ukaa na kukuwa kiuchumi“
Na Betold Chove- Katavi
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema katika juhudi za utunzaji wa mazingira mkoa umetenga misitu 30 kwa ajili ya kuhifadhi na kuingia kwenye biashara ya kaboni.
Mwanamvua ameyasema hayo mbele ya Waziri wa Nchi (Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Saidi Jafo katika kikao kilichofanyika katika ofisi za jengo la Mkuu wa Mkoa wakati akisoma taarifa ya mwelekeo wa mkoa katika kuchangamkia fursa za kimazingira na mafanikio yaliyopatikana hadi sasa katika halmashauri ya Tanganyika baada ya vijiji 8 kunufaika na mradi wa Kaboni.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza mbele ya waziri Jafo
Kwa upande wake waziri wa nchi (muungano na mazingira, Dkt.Selemani Saidi Jafo akizungumza amezitaka halmashauri zote mkoani Katavi kutunza mazingira ili waweze kunufaika na biashara ya hewa ya ukaa ili kuongeza mapato kupitia biashara hiyo.
Sauti ya Waziri wa Nchi (Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Saidi Jafo akizungumza na wananchi
Waziri wa Nchi (Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Saidi Jafo .picha na site tv