Katavi: Watoto waendelea kuogelea mto Misunkumilo
24 May 2024, 10:05 am
“Serikali ya mtaa haitasita kuchukua hatua kwa wazazi ambao watoto wao watabainika wanazurura mtaani, amesema mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda Hoteli Christina Mshani” Picha na Samwel Mbugi
Wazazi Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kutimiza wajibu Wa kuwalinda watoto wasiogelee kwenye mto Minsukumilo ili athari hasi zinasosababishwa na mto huo ikiwemo video visiweze kutoka.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda hoteli Christina Mshani wakati akizungumza na Mpanda Radio FM ambapo amesema ni wajibu wa jamii kushiriki katika kuwalinda watoto dhidi ya hatari mbalimbali Kwakuwa wazazi wamekuwa wakiwaona watoto wakiogelea mtoni hapo bila kuwakanya.
Aidha Mshani amesema serikali ya mtaa huo haitasita kuchukua hatua kwa wazazi ambao watoto wao watabainika wanazurura mtaani.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi wakizungumza na kituo hiki wamesema kuwa kutokana na majukumu ya maisha imepelekea kutoka kutafuta ridhiki na kuwaacha watoto majumbani bila uangalizi wa uhakika jambo ambalo limechangia kuwapa uhuru watoto kutoroka na kuelekea maeneo mbalimbali kwenye michezo ikiwemo Kuogelea Katika mto misunkumilo.
Ikumbukwe kuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka 2023 mtoto mmoja alizama wakati akiogelea Katika mto misunkumilo licha ya juhudi za kumtafuta hazikufanikiwa Bado watoto wameendelea kuchezea Katika madimbwi ya mto huo.