Katavi kunufaika na mashine mpya kunusuru kukatika umeme
20 May 2024, 3:46 pm
Na mwandishi wetu Dodoma
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema mradi wa ujenzi wa njia ya umeme kutoka Tabora hadi Katavi wenye thamani ya shilingi bilioni 116 umefikia asilimia 58, ambapo utakapokamilika utauunganisha mkoa wa Katavi kwenye gridi ya taifa.
Naibu Waziri Judith Kapinga ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi aliyetaka kujua ni lini mradi huo utakamilika.
Katika swali lake la msingi mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Mh. Sebastian Kapufi alitaka kujua ni lini mradi huo utakamilika ili kuondoa changamoto ya umeme katika mji wa Mpanda na pia mkakati madhubuti wa serikali ili kuunusuru mji wa Mpanda dhidi ya kukatika kwa umeme mara kwa mara jambo linalosababisha kazi za uzalishaji kwa kutumia nishati ya umeme kusimama.
Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amesema mradi wa ujenzi wa njia ya umeme kutoka Tabora hadi Katavi wenye thamani ya shilingi Bilioni 116 umefikia asilimia 58, ambapo utakapokamilika utauunganisha mkoa wa Katavi kwenye gridi ya Taifa.
Kuhusu mpango wa kunusuru kukatika umeme wakati mradi huo ukiendelea ameagiza mafundi kufungua mtambo wa Megawatt 1 katika wilaya ya biharamuro na kuupekeka katika mji wa Mpanda ili kuhakikisha unapunguza changamoto ya KuKata lwa umeme.
Hivi karibuni baraza la madiwani halmashauri ya Manispaaya Mpanda walipokutana waliomba kuongezewa mashine ambayo itapunguza changamoto ya kukatika kwa umeme ili shunguli za uzalishaji ziweze kuendelea.