Mpanda FM

Mpanda Madiwani WaivaaTanesco Umeme Kukata Mara kwa Mara

15 May 2024, 11:59 pm

Kukatika kwa umeme baadhi ya maeneo imekuwa inajirudia na kumekuwa hakuna taarifa kutoka mamlaka husika jambo ambalo limekuwa likipeekea changamoto ya kusimama kwa baadhi ya kazi za watu zinazotegemea nishati ya umeme” Picha na Lilian Vicent

Na Lilian Vicent-Katavi

Wananchi wa maeneo mbalimbali mkoani katavi wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya kukatika  kwa umeme ghafla  bila ya kutolewa kwa taarifa  kwa umma na TANESCO.

Hayo yamesemwa  na diwani wa kata ya kashaulili Magret Kitungulu wakati akiuliza swali kufuatia  taarifa iliyowasilishwa na TANESCO mkoani hapa katika kikao robo ya tatu cha baraza la madiwani  na ameongeza kuwa kukatika kwa umeme baadhi ya maeneo imekuwa inajirudia na kumekuwa hakuna taarifa kutoka mamlaka husika jambo ambalo limekuwa likipeekea changamoto ya kusimama kwa baadhi ya kazi za watu zinazotegemea nishati ya umeme.

Sauti ya Diwani wa kata ya kashaulili Magret Kitungulu wakati akiuliza swali kufuatia  taarifa iliyowasilishwa na TANESCO

Kwa upande wake Afisa masoko mkuu TANESCO Proches Joseph amesema kuwa amepokea suala hilo  watajihatihidi kuandaa ratiba itayosaidia watu kufahamu na shughuli zingine ziweze kuendelea.

Sauti ya Afisa masoko mkuu TANESCO Proches Joseph akijibia changamoto hiyo.

Nae mstahiki meya  Haidary Sumry kwa niaba ya baraza hilo amewasilisha ombi kwa naibu waziri mkuu ambaye  waziri wa nishati dotto biteko  kuongezewa mashine kwaajili ya kuondoa changamoto ya upungufu wa umeme.

Sauti ya mstahiki meya  Haidary Sumry kwa niaba ya baraza hilo akiwasilisha ombi kwa naibu waziri mkuu nishati dotto biteko  kuongezewa mashine.

Mstahiki meya  Haidary Sumry alipokuwa akiongoza baraza la madiwani. Picha na Lilian Vicent