Waumini wilayani Tanganyika watakiwa kumjua Mungu ili kutokomeza vitendo vya ukatili
15 May 2024, 10:07 am
Waumini wa makanisa mbalimbali wiliojetokeza katika kongamano.picha na Samwel Mbugi
“Wanapaswa kusoma vitabu vya neno la Mungu ili kumjua Mungu na kuepukana na vitendo vya ukatili kutokana na kuwa na hofu ya Mungu“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Waumini wa makanisa mbalimbali wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wametakiwa kumjua Mungu kwa kupitia maandiko ya kibiblia na vitabu mbalimbali ili kutokomeza ukatili katika jamii
Hayo yamesema na mkurugenzi mkuu wa huduma ya TNI afrika Mashariki Annette Mtui wakati wa uzinduzi wa kitabu cha RHAPSODI katika viwanja vya Ilebula B Kijiji cha Kamsanga kuwa kuna umuhimu wa kusoma maandiko ya vitabu mbalimbali.
Sauti ya mkuu wa huduma ya TNI afrika Mashariki Annette Mtui
Kwa upande wa diwani wa kata ya Mnyagalla Macklasi Cosmas Nyanda ambae alikuwa mgeni mwalikwa ametoa shukrani kwa waandaji wa kongamano hilo ambapo amesema wameweza kupata elimu mbalimbali ambayo itawasaidia wananchi
Sauti ya diwani wa kata ya Mnyagalla Macklasi Cosmas Nyanda
Nae mgeni rasmi Saidi Wambali ambae amemwakilisha Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Moshi Seleman Kakoso amesema kuwa elimu watakayoipata kupitia kitabu hicho itawasaidia kuwa na maadili kwa baadhi ya wananchi ambao walikuwa hawana Imani ya kiroho.
Sauti ya mgeni rasmi Saidi Wambali ambae amemwakilisha Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Moshi Seleman Kakoso
Hata hivyo amewataka wananchi ambao wamepata kitabu hicho kuendelea kusoma kwana kitakuwa ni mkombozi kwa baadhi ya vijana na jamii kwa ujumla kuwa na hofu ya Mungu.
Waumini waliojitokeza katika kongamano hilo.picha na Samwel Mbugi