Mpanda FM

Jengo la kusafisha damu Katavi kukamilika Juni 2024

3 May 2024, 2:56 pm

Muonekano wa jengo la kusafishia damu ambalo linajengwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi. “Picha na Gladness Richard”

“Kukamilika kwa jengo hilo litaondoa adha ya changamoto ya wananchi kupata huduma hiyo mikoa mingine na kuwasaidia kupata huduma hiyo hapa mkoani Katavi”

Na Gladness Richard-Katavi

Zaidi ya milioni 100.96 zimetumika kujengea  jengo la kusafishia damu ambalo linajengwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi .

Akisoma taarifa ya mradi huo msanifu wa majengo kutoka katika hospital ya rufaa ya mkoa wa katavi   Aggrey Ndimbo amesema kuwa mradi huo unatarajia kukamilika ifikapo tarehe 10/7/2024.

Sauti ya msanifu wa majengo kutoka katika hospital ya rufaa ya mkoa wa katavi   Aggrey Ndimbo akisoma taarifa ya ujenzi.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema kuwa ujenzi huo unatakiwa kukamilika kwa wakati huku akiwataka  viongozi wa hospitali kuruhusu vifaa vyote vilivyopo stoo vifunguliwe na kuanza kutumika.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko akitoa maelekezo alipotembelea kukagua ujenzi wa mradi huo

Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko alipotembelea kukagua ujenzi wa mradi huo. Picha na Gladness Richard

Kukamilika kwa jengo hilo litaondoa adha ya changamoto ya wananchi kupata huduma hiyo mikoa mingine na kuwasaidia kupata huduma hiyo hapa mkoani