Waendesha bodaboda mkoani Katavi wapaza sauti zao kuhitaji uchaguzi
1 May 2024, 11:25 pm
picha na mtandao
“Tunasababishiwa ajali ,tunagongwa na Magari bodaboda tunapigwa ,tunanyanyasika “
Na Lilian Vicent -Katavi
Waendesha bodaboda mkoani Katavi Wametaka kufanyika kwa uchaguzi wasafu ya uongozi wa boda boda mkoani hapa kutokana na uongozi uliopo madarakani kushindwa kuwatatulia matatizo yanayowakabili.
Wameyasema hayo wakati wa kikao cha kusikiliza kero wanazokumbana nazo madereva bodaboda katika ukumbi wa Polisi Club na kusema kuwa baadhi yao wamekuwa wakipigwa viboko na askari wa ulinzi shirikishi.
sauti za madereva bodaboda wakizungumza juu ya changamoto wanazopitia
Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Kaster Ngonyani amesema amesikiliza kero hizo na atazifanyia utatuzi na kueleza uchaguzi wa kuchagua wa viongozi wapya wa bodaboda utafanyika tarehe 01 mwezi wa Sita mwaka huu.
Sauti ya Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Kaster Ngonyani akizungumza
Naye mwenyekiti wa bodaboda mkoani hapa Andrea Mwakalambo ameeleza kuwa hajawahi kufuatwa na bodaboda yeyote kudai uchaguzi na kama wanahitaji hivyo ni vyema kufuata utaratibu.
Sauti ya Mwenyekiti wa bodaboda mkoa wa Katavi