Katavi: Ombi la rufaa lakubaliwa kutofukuliwa mwili wa Bukuku
29 April 2024, 7:05 pm
“Wazazi wa marehemu Lwitiko hawatambua kama mtoto wao huyo aliwahi kubadili dini na kuwa mwislam“
Na Samwel Mbugi-Katavi
Familia ya marehemu aliyefahamika kwa jina la Lwitiko Bukuku imeiomba mahakama kutenda haki katika kesi iliyofunguliwa na anayejieleza kuwa ni mke wa marehemu akidai mumewe amezikwa kwa imani ya dini ya Kikristo badala ya imani ya Kiislamu.
Hayo yamesemwa na dada na kaka wa marehemu Mary Bukuku na Edward Bukuku wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm kuwa kesi hiyo imeleta taharuki kwa ndugu na jamaa kwani wao kama familia hawakujua kama marehemu alikuwa amebadili dini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mnazi mmoja Mussa Alfani amesema kuwa tarifa za ufukuaji wa kabuli ni za kweli na zilileta taharuki kwa wanachi wa mtaa huo kwani tukio hilo ni mara ya kwanza kutokea katika mtaa wake.
Pia Mussa amewataka wananchi wanaomzushia kuwa ameegemea upande mmoja waache mara moja kwani yeye anasimamia haki ya kila mwananchi wa mtaa wake tofauti na wanavyofikilia kuwa yuko upande wa familia ya marehemu.
Hata hivyo Mahakama ya wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi imekubali ombi la rufaa kwa ndugu wa marehemu ambayo imesikilizwa Aprili 29, 2024 ya zuio la kufukua mwili wa marehemu ambapo ulipaswa kufukuliwa na kuzikwa upya kwa imani ya dini ya Kiisilam ,na kesi hiyo itapangwa tarehe ya kusikiliza tena.