DC Mpanda aagiza kufanyika tathmini maafa ya mafuriko
14 April 2024, 2:18 pm
Baadhi ya Nyumba zikiwa zimezingirwa na Maji katika Kata ya Misunkumilo .Picha na Restuta Nyondo
“Baada ya kupata taarifa amefika eneo la tukio na kuanza kuchukua hatua za awali ili kuwanusuru wananchi “
Na Betold Chove-Katavi
Mkuu wa wilaya Ya Mpanda Jamila Yusuph Ameziagiza Kamati za Maafa halmashauri ya Nsimbo na Mpanda kufanya Tathimini ya Mafuriko yaliyotokea kufuatia Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamikia April 14 na kusababisha Mafuriko kwa baadhi ya Nyumba Misunkumilo.
Akizungumza alipofika Daraja la Mto Misunkumilo kushuhudia Madhara yaliyojitokeza baada ya Mvua hizo kunyesha na kusababisha kukatisha Mawasiliano ya Barabara kuu inayotoka Mpanda kuelekea mkoani Kigoma baada ya Maji kujaa na kupita juu ya Daraja.
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akizungumza juu ya Maafa hayo
Kwa upande wao Wananchi waliokumbwa na Mafuriko hayo wameeleza namna walivyoathirika na mafuriko hayo na kuzitaka Mamlaka kuwasaidia ili waweze kuendelea na Shughuli za Maendeleo.
Sauti za Wananchi wakieleza namna Mafuriko yalivyowaathiri
Diwani wa kata ya Misunkumilo Alfred atondo Akizungumza na Mpanda Redio Fm amesema kuwa mara baada ya kupata Taarifa amefika eneo la Tukio na kuanza kuchukua hatua za awali ili kuwanusuru Wananchi wake
Sauti ya Diwani wa Kata ya Misunkumilo akieleza hatua alizozichukua kufuatia Mafuriko hayo
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wiaya ya Mpanda amewataka Wananchi wanaoshi kando ya Mito kuchukua tahadhari na kuhama pia kuwataka kutoa taarifa wote walioathirika na Mafuriko ili kuisadia kamati ya Maafa athari za mafuriko ili Serikali iweze kutoa Msaada.
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda akiwataka wananchi kutoa taarifa kwa wakati dhidi ya Maafa yanayojitokeza